skip to Main Content
+255 713 860 515 / +255 767 860 515 tuliatrust.org@gmail.com
TULIA TRADITIONAL DANCE FESTIVAL 2021 KUFANYIKA SEPTEMBA 23-25 JIJINI MBEYA.

TULIA TRADITIONAL DANCE FESTIVAL 2021 KUFANYIKA SEPTEMBA 23-25 JIJINI MBEYA.

Mashindano ya Ngoma za Asili maarufu kama TULIA TRADITIONAL DANCE FESTIVAL 2021 yanatarajiwa kufanyika Jijini Mbeya tarehe 23-25 Mwezi wa Tisa Mwaka huu katika Viwanja vya Airpot ya Zamani Kata ya Iyela.

Hii ni mara ya tano kufanyika shindano hili la ngoma za asili tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2016 na yalikuwa yakifanyika Wilayani Rungwe yakiwa na lengo la kukuuza na kuuenzi utamaduni wetu ambapo vikundi mbalimbali vya ngoma za asili zaidi ya 100 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania vitashindana na kupatikana washindi.

Tulia Trust inawakaribisha Wadau mbalimbali wa Sanaa Kushiriki kwa namna mbalimbali ikiwemo kudhamini mashindano haya yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni na kuwa sehemu ya kukuza utamaduni wetu wa asili.

Kwa Mawasiliano zaidi Piga +255-767-860-515 na +255-752-668-006

Changia Kupitia CRDB Bank: 0150226766000

 

 

Back To Top
Search