skip to Main Content
+255 713 860 515 / +255 767 860 515 tuliatrust.org@gmail.com
ZAIDI YA MILIONI 21.4 ZIMETUMIKA KUWAWEZESHA VIJANA JIJINI MBEYA

ZAIDI YA MILIONI 21.4 ZIMETUMIKA KUWAWEZESHA VIJANA JIJINI MBEYA

June 28,2021 Taasisi ya Tulia Trust tumeendelea kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kutoa mkopo wa Pikipiki 9 kwa vijana wa Bodaboda Kanda ya Uyole Jijini Mbeya wenye thamani ya shilingi milioni 21.4.

Akikabidhi mkopo huo kwenye ofisi za  Kanda ya Uyole Meneja wa Tulia Trust Jacqueline Boaz amesema lengo la Taasisi ni kuwawezesha vijana kiuchumi ,mbali ya bodaboda Taasisi hukopesha pia pikipiki za miguu mitatu(Bajaj) na pesa taslim.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Aliko Fwanda ameishukuru Taasisi ya Tulia Trust kuwawezesha mikopo ya pikipiki ambapo mpaka sasa wamekopeshwa pikipiki zaidi ya 80 ambapo hurejesha kidogokidogo,Kwa upande wake Frank Tebro Mwenyekiti wa Kanda ya Uyole amesema mkopo huo wataulipa kwa wakati na Taasisi iendelee kuwakopesha.
Nao baadhi ya wanufaika wa mkopo huo Deligo Kunzugala amesema mikopo inayotolewa na Taasisi ya Tulia Trust haina urasimu.
Taasisi ya Tulia Trust mbali ya kutoa mikopo ya Pikipiki na Bajaj pia hutoa misaada kijamii kama miundombinu ya elimu,afya,michezo,ngoma na mikopo ya fedha ikiwa ni kurejesha fadhila kwa jamii.

 

Back To Top
Search